sw_jhn_text_reg/20/11.txt

1 line
393 B
Plaintext

\v 11 Hata hivyo, Mariamu alikuwa amesimama nje ya kaburi akilia, alivyokuwa akiendelea kulia aliinama kisha akatazama kaburini. \v 12 Akaona malaika wawili waliovalia mavazi meupe wamekaa mmoja kichwani na mwingine miguuni mahali ambapo Yesu alikuwa amelala. \v 13 Nao wakamwambia, "Mwanamke, kwa nini unalia?" Naye akawaambia, "Ni kwa sababu wamemchukua Bwana wangu, nami sijui walikomweka."