sw_jhn_text_reg/19/40.txt

1 line
442 B
Plaintext

\v 40 Kwa hiyo wakauchukua mwili wa Yesu wakaufanga kwenye sanda ya kitani na pamoja na yale manukato, kama ilivyokuwa desturi ya wayahudi wakati wa kuzika. \v 41 Mahali ambapo Yesu alisulibiwa kulikuwa na bustani; ndani ya ile bustani kulikuwa na kaburi jipya ambalo hakuna mtu alikuwa amawahi kuzikwa humo. \v 42 Basi, kwa kuwa ilikuwa siku ya maandalio kwa Wayahudi, na kwa vile lile kaburi lilikuwa karibu, basi wakamlaza Yesu ndani yake.