sw_jhn_text_reg/19/04.txt

1 line
481 B
Plaintext

\v 4 Kisha Pilato alitoka nje na kuwaambia watu, "Tazama nawaleteeni huyu mtu kwenu ili mjue kwamba mimi sikuona hatia yoyote ndani yake." \v 5 Kwa hiyo Yesu akatoka nje; alikuwa amevaa taji ya miiba na vazi la zambarau. Ndipo Pilato akawaambia, "Tazameni mtu huyu hapa!" \v 6 Kwa hiyo wakati kuhani mkuu na wakuu walipomwona Yesu, wakapiga kelele wakisema, "Msulubishe, msulubishe." Pilato akawaambia, "Mchukueni ninyi wenyewe mkamsulubishe, kwa kuwa mimi sioni hatia ndani yake."