sw_jhn_text_reg/18/01.txt

1 line
465 B
Plaintext

\c 18 \v 1 Baada ya Yesu kusema maneno haya, aliondoka na wanafunzi wake kuelekea upande wa pili wa kijito cha Kidron, ambako kulikuwa na bustani, ambamo yeye na wanafunzi wake waliingia. \v 2 Sasa yule Yudasi, aliyekuwa amsaliti,alilijua eneo hilo, kwani Yesu alikuwa akikutana hili eneo mara kwa mara akiwa na wanafunzi wake. \v 3 Naye Yudasi, baada ya kuwa amepata kundi la maaskari na maofisa toka kwa wakuu wa makuhani, wakaja wakiwa na taa, kurunzi na silaha.