sw_jhn_text_reg/17/09.txt

1 line
404 B
Plaintext

\v 9 Ninawaombea wao. Siuombei ulimwaengu bali wale ulionipa kwa kuwa wao ni wako. \v 10 Vitu vyote ambavyo ni vyangu ni vyako, na vile ulivyonavyo wewe ni vyangu; nami ninatukuzwa katika hivyo. \v 11 Mimi simo tena ulimwenguni, bali wao wamo ulimwenguni, nami sasa naja kwako. Baba Mtakatifu, watunze kwa jina lako lile ulilonipa mimi ili wao nao wawe kitu kimoja, kama vile mimi na wewe tu kitu kimoja.