sw_jhn_text_reg/16/22.txt

1 line
339 B
Plaintext

\v 22 Ninyi pia mna huzuni sasa, lakini nitawaona tena; na mioyo yenu itafurahi na hakuna atakayeweza kuiondoa furaha yenu. \v 23 Siku hiyo hamtaniuliza lolote. Amin, Amin, nawaambia, Mkiomba lolote kwa Baba, atawapa kwa jina langu. \v 24 Mpaka sasa hamjaomba lolote kwa jina langu; ombeni, nanyi mtapokea ili kwamba furaha yenu itimilike.