sw_jhn_text_reg/16/19.txt

1 line
528 B
Plaintext

\v 19 Yesu aliona kuwa walitamani kumuuliza, naye akawaambia, "Mnajiuliza wenyewe kuhusu hili, nilivyosema, 'Bado muda mfupi, hamtaniona tena; na baada ya muda mfupi mtaniona'? \v 20 Amin, amin, nawaambia, mtalia na kuomboleza, lakini ulimwengu utashangilia, mtakuwa na huzuni lakini huzuni yenu itageuka kuwa furaha. \v 21 Mwanamke anakuwa na huzuni wakati anapokuwa na uchungu kwa sababu wakati wa kujifungua umefika; lakini anapojifungua mtoto, hakumbuki tena maumivu kwa sababu ya furaha yake kwamba mtoto amezaliwa duniani.