sw_jhn_text_reg/13/36.txt

1 line
385 B
Plaintext

\v 36 Simoni Petro alimwambia, "Bwana, unakwenda wapi?" Yesu akajibu, "Mahali ninapokwenda kwa sasa hutaweza kunifuata, lakini utanifuata baadaye." \v 37 Petro akamwambia, "Bwana, kwa nini nisikufuate hata sasa? Mimi nitayatoa maisha yangu kwa ajili yako." \v 38 Yesu akajibu, "Je utayatoa maisha yako kwa ajili yangu? Amini amini nakwambia, jogoo hatawika kabla hujanikana mara tatu."