sw_jhn_text_reg/13/28.txt

1 line
339 B
Plaintext

\v 28 Sasa hakuna mtu katika meza alijua sababu ya Yesu kusema jambo hili kwake. \v 29 Baadhi yao walidhani kwamba, kwa sababu Yuda alishika mfuko wa fedha, Yesu alimwambia, "Nunua vitu tunavyohitaji kwa ajili ya sikukuu," au kwamba anapaswa kutoa kitu kwa masikini. \v 30 Baada ya Yuda kupokea mkate, alitoka nje haraka; na ilikuwa usiku.