sw_jhn_text_reg/12/27.txt

1 line
373 B
Plaintext

\v 27 Sasa roho yangu imefadhaika: nami nisemeje? 'Baba, uniokoe katika saa hii'? Lakini ni kwa kusudi hii nimeifikia saa hii. \v 28 Baba, litukuze jina lako." Kisha sauti ikaja kutoka mbinguni na kusema, "Nimelitukuza na nitalitukuza tena." \v 29 Basi mkutano uliosimama karibu naye wakasikia, wakasema ya kwamba kumekuwa ngurumo. Wengine walisema, "Malaika amesema naye."