sw_jhn_text_reg/12/01.txt

1 line
469 B
Plaintext

\c 12 \v 1 Siku sita kabla ya Pasaka, Yesu alienda Bethania, alipokuwapo Lazaro, yeye ambaye alimfufua kutoka katika wafu. \v 2 Basi wakamwandalia chakula cha jioni huko, na Martha akawatumikia, wakati huo Lazaro alikuwa mmoja wapo wa wale walioketi mezani pamoja na Yesu. \v 3 Kisha Mariamu akachukua ratli ya manukato yaliyotengenezwa kwa nardo safi, yenye thamani kubwa, akampaka Yesu miguuni, na kumfuta miguu kwa nywele zake; nyumba yote ilijaa harufu ya manukato.