sw_jhn_text_reg/08/42.txt

1 line
501 B
Plaintext

\v 42 Yesu akawaambia, "Ikiwa Mungu ni Baba yenu, mngenipenda mimi,maana nimetoka kwa Mungu; wala sikuja kwa nafsi yangu, bali yeye alinituma. \v 43 Kwa nini hamyaelewi maneno yangu? Kwa sababu hamuwezi kuvumilia kuyasikia maneno yangu. \v 44 Ninyi ni wa baba yenu, shetani, na mnataka kuzitenda tamaa za baba yenu. Alikuwa mwuaji tangu mwanzo na hawezi kusimama katika kweli kwa sababu kweli haimo ndani yake. Anapoongea uongo, anaongea kutoka kwenye asili yake kwa sababu ni mwongo na baba wa uongo.