sw_jhn_text_reg/04/34.txt

1 line
367 B
Plaintext

\v 34 Yesu akawambia, "Chakula changu ni kufanya mapenzi yake yeye aliyenituma na kutimiza kazi yake. \v 35 Je, hamsemi, 'Bado miezi minne na mavuno yatakuwa tayari?' Ninawambieni tazameni mashamba yalivyo tayari kwa mavuno! \v 36 Yeye avunaye hupokea mishahara na kukusanya matunda kwa ajili ya uzima wa milele, ili kwamba yeye apandaye naye avunaye wafurahi pamoja.