\v 5 Palikuwa na mtu mmoja aliyekuwa ameugua kwa muda wa miaka thelathini na minane ndani ya matao. \v 6 Yesu alipomwona amelala ndani ya matao na baada ya kutambua kuwa amelala pale kwa muda mrefu Yesu alimwambia, "Je unataka kuwa mzima?"