\v 17 Akamwambia tena mara ya tatu, "Simon, mwana wa Yohana, Je wanipenda?" Naye Petro alihuzunika kwa vile alivyomwambia mara ya tatu, "Je Wewe wanipenda?" Naye akamwambia, "Bwana, unajua yote; unajua kuwa nakupenda." Yesu akamwambia, Lisha kondoo wangu. \v 18 Amini, amini, nakuambia, ulipokuwa kijana ulizoea kuvaa nguo mwenyewe na kwenda kokote ulikotaka; lakini utakapokuwa mzee, utanyosha mikono yako, na mwingine atakuvalisha nguo na kukupeleka usikotaka kwenda."