\v 10 Yesu akawambia, "Leteni baadhi ya samaki mliovua sasa hivi." \v 11 Basi Simon Petro akapanda na kuukokota ule wavu uliokuwa umejaa samaki wakubwa, kiasi cha samaki 153; japo walikuwa wengi, ule wavu haukuchanika.