\v 7 Wayahudi wakamjibu Pilato, "Sisi tunayo sheria, na kwa sheria hiyo inampasa kufa kwa sababu yeye alijifanya kuwa mwana wa Mungu." \v 8 Pilato aliposikia maneno haya alizidi kuogopa, \v 9 akaingia Praitorio tena na kumwambia Yesu, "Wewe unatoka wapi? Hata hivyo, Yesu hakumjibu.