\v 3 Huu ndio uzima wa milele: kwamba wakujue wewe, Mungu wa kweli na wa pekee, na yeye uliyemtuma, Yesu Kristo. \v 4 Nimekutukuza hapa duniani, na kuikamilisha kazi uliyonipa niifanye. \v 5 Sasa, Baba, unitukuze mimi pamoja na wewe mwenyewe kwa utukufu ule niliokuwa nao pamoja na wewe kabla ya ulimwengu kuumbwa.