\c 17 \v 1 Yesu alipoyasema mambo haya; akainua macho yake kuelekea mbinguni na akasema, "Baba, saa imewadia; mtukuze mwanao ili na mwana naye akutukuze wewe - \v 2 kama vile ulivyompatia mamlaka juu ya vyote vyenye mwili ili awape uzima wa milele wale wote uliompatia.