\v 12 Ninayo mengi ya kuwaambia, lakini hamtayaelewa sasa. \v 13 Lakini, yeye, Roho wa kweli, akija, atawaongoza katika kweli yote; kwa kuwa hataongea kwa ajili yake mwenyewe; lakini yoyote atakayoyasikia, atayasema mambo hayo; na atawambieni mambo yatakayokuja. \v 14 Yeye atanitukuza mimi, kwa sababu atayachukua mambo yangu na atayatangaza kwenu.