\v 3 Watawatendea mambo haya kwa sababu hawamfahamu Baba wala Mimi. \v 4 Nimewaambia mambo haya ili kwamba wakati wa haya kutokea ukifika, mtakumbuka jinsi nilivyowaambia kuyahusu. Sikuwaambia kuhusu mambo haya tangu mwanzo kwa sababu nilikuwa pamoja nanyi.