\v 23 Anichukiaye mimi humchukia Baba yangu pia. \v 24 Ikiwa sijafanya kazi miongoni mwao ambayo hapana mmoja aliyeifanya, wangelikuwa hawana dhambi; lakini sasa wamefanya yote mawili wameona na wamenichukia mimi na Baba yangu. \v 25 Hili linatokea ili kwamba neno litimie ambalo limeandikwa katika sheria yao: 'Wananichukia mimi bila sababu.'