\v 5 Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi. Yeyote anayedumu ndani yangu na mimi ndani yake,yeye huzaa matunda mengi, kwa kuwa pasipo mimi hamuwezi kufanya jambo lolote. \v 6 Ikiwa mtu yeyote hatasalia ndani yangu, hutupwa kama tawi na kukauka; watu hukusanya matawi na kuyatupa katika moto, na kuteketea. \v 7 Ikiwa mtadumu ndani yangu, na kama maneno yangu yakidumu ndani yenu, ombeni lolote mtakalo, nanyi mtafanyiwa.