\v 25 Yeye apendaye uhai wake ataupoteza; bali yeye auchukiaye uhai wake katika ulimwengu huu atausalimisha hata uzima wa milele. \v 26 Mtu yeyote akinitumikia mimi; na anifuate; nami nilipo, ndipo na mtumishi wangu atakapokuwapo. Mtu yeyote akinitumikia, Baba atamheshimu.