\v 8 Wanafunzi wakamwambia, "Rabi, Wayahudi walikuwa wakijaribu kukupiga mawe, na wewe unataka kurudi huko tena?" \v 9 Yesu akawajibu, "Saa za mchana si kumi na mbili? Mtu anapotembea mchana hawezi kujikwaa, kwa sababu anaona kwa mwanga wa ulimwengu huu.