\v 25 Kwa hiyo wakamwambia, "Wewe ni nani?" Yesu akawaambia, Yale niliyowaambia tangu mwanzo. \v 26 Ninayo mambo mengi ya kuzungumza na kuhukumu juu yenu. Hata hivyo, yeye aliyenituma ni wa kweli; na mambo niliyoyasikia kutoka kwake, mambo haya nayasema kwa Ulimwengu." \v 27 Hawakumuelewa kwamba alikuwa akiongea nao kuhusu Baba.