\v 21 Basi akawaambia tena, "Ninaenda zangu; mtanitafuta na mtakufa katika dhambi zenu. Kule niendako, hamuwezi kuja." \v 22 Wayahudi wakasema, "Atajiua mwenyewe, maana anasema,'kule niendako hamuwezi kuja'?"