\v 14 Yesu alijibu akawaambia, "Hata kama najishuhudia mwenyewe, ushuhuda wangu ni kweli. Ninajua mahali nilikotoka na kule ninakoenda, lakini ninyi hamjui mahali ninapotoka au kule niendako. \v 15 Nyinyi mnahukumu kimwili; mimi simhukumu yeyote. \v 16 Mimi hata nikihukumu, hukumu yangu ni kweli kwa sababu siko peke yangu, bali niko pamoja na baba aliyenituma.