\v 1 Mwanzoni kulikuwako Neno, na Neno alikuwa pamoja na Mungu, na Neno alikuwa Mungu. \v 2 Huyu, Neno, Mwanzoni alikuwa pamoja na Mungu. \v 3 Vitu vyote vilifanyika kupitia yeye, na pasipo yeye hakuna hata kitu kimoja kilichokuwa kimefanyika.