sw_jer_text_reg/24/04.txt

1 line
498 B
Plaintext

\v 4 Ndipo neno la Bwana likanijia, kusema, \v 5 "Bwana, Mungu wa Israeli, asema hivi: nitawaangalia mateka wa Yuda kwa manufaa yao, kama vile tini hizi nzuri, nilipowatoa mateka kutoka hapa mpaka nchi ya Wakaldayo. \v 6 Nitaweka macho yangu kwao wapate mema na kuwarejeshea nchi hii. Nitawajenga, wala sitawaangamiza. \v 7 Nitawapanda, wala sitawang'oa. Ndipo nitawapa moyo wa kunijua; kwa kuwa mimi ndimi Bwana. Watakuwa watu wangu na mimi nitakuwa Mungu wao, hivyo watanirudia kwa moyo wao yote.