sw_jer_text_reg/43/11.txt

1 line
519 B
Plaintext

\v 11 Kwa kuwa atakuja na kuvamia nchi ya Misri. Yeyote aliyeandikiwa kifo atakufa. Yeyote aliyeandikiwa mateka atachukuliwa mateka. Na yeyote aliyeandikiwa kwa upanga atakufa kwa upanga. \v 12 Kisha nitawasha moto katika mahekalu ya miungu ya Misri. Nebukadreza atawachoma au kuwateka. Atasafisha nchi ya Misri kama wachungaji wanavyosafisha wanyama waharibuo nguo zao. Ataenda nje kutoka eneo hilo kwa ushindi. \v 13 Atavunja nguzo za mawe huko Heliopolisi kwenye nchi ya Misri. Atachoma mahekalu ya miungu ya Misri."