sw_jer_text_reg/07/21.txt

1 line
466 B
Plaintext

\v 21 BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli asema hivi, Jiongezeeni sadaka za kuteketezwa katika dhabihu zenu na nyama zake. \v 22 Kwani wakati nilipowatoa mababu zenu kutoka nchi ya Misri, Sikuhitaji chochote kutoka kwao. Sikuwapa amri juu ya maswala ya sadaka za kuteketezwa na dhabihu. \v 23 Niliwapa amri hii tu, "Sikilizeni sauti yangu, nami nitakuwa Mungu wenu nanyi mtakuwa watu wangu. Kwa hiyo muishi katika njia ambazo ninawaamuru, ili mambo yenu yawe mazuri."