sw_jer_text_reg/04/27.txt

1 line
457 B
Plaintext

\v 27 Hiki ndicho BWANA asemacho, "Nchi yote itakuwa uharibifu, lakini sitawaharibu wote kabisa. \v 28 Kwa sababu hii nchi itaomboleza, na mbingu juu zitatiwa giza. Kwa kuwa nimesema haya na kuyakusudia; sitarudi nyuma; Sitaacha kuyatekeleza. \v 29 Kila mji utakimbia kutoka katka kelele za wapandafarasi na wenye pinde; Watakimbilia msituni, Kila mji utapanda hadi mahali pa miamba. Miji itatelekezwa, kwa kuwa hakutakuwa na mtu wa kuishi katika miji hiyo.