sw_jer_text_reg/03/13.txt

1 line
434 B
Plaintext

\v 13 Kiri uovu wako, kwa kuwa umefanya dhambi dhidi ya BWANA, Mungu wako; umemshirikisha njia zako mgeni chini ya kila mti wenye majani mabichi! wala hukuisikiliza sauti yangu! - asema BWANA. \v 14 Rudini, enyi watu waasi! - asema BWANA - kwa kuwa mimi nimekuoa wewe! Nitakurudisha wewe mmoja katika mji, wawili katika ukoo mmoja, na nitawarudisha Sayuni! \v 15 Nitawapa wachungaji niwapendao, na watawachunga kwa maarifa na ufahamu.