sw_jer_text_reg/02/04.txt

1 line
531 B
Plaintext

\v 4 Sikilizeni neno la BWANA, enyi nyumba ya Yakobo na kila familia katika nyumba ya Israeli. \v 5 BWANA anasema hivi, "Ni makosa gani ambayo baba zenu waliyaona kwangu, hata wakatae kunifuata mimi? hata wazifuate sanamu ambazo hazina chochote na wao kuwa si kitu? \v 6 Wala hawakusema, BWANA yuko wapi, ambaye alitutoa katika nchi ya Misri? BWANA yuko wapi, ambaye alituongoza katika jangwa, katika nchi ya Araba na mashimo, katika nchi ya ukame na giza nene, katika nchi ambayo hakuna mtu apitaye wala hakuna mtu anayeishi humo?