sw_jer_text_reg/46/07.txt

1 line
407 B
Plaintext

\v 7 Ni nani hawa wainukao kama Nile, ambao maji yao yanaruka juu na chini kama mito? \v 8 Misri huinuka kama mto Nile, na maji yake yanaumuka juu na chini kama mito. Anasema, 'nitapanda juu; nitaifunika nchi. Nitaiharibu miji na watu wake. \v 9 Inukeni, farasi. Mwe na hasira, ninyi vibandawazi. Askari na waende, Kushi na Putu, watu walio na ujuzi wa ngao, na Ludimu, watu wenye ujuzi wa kupiga pinde zao.