sw_jer_text_reg/27/01.txt

1 line
792 B
Plaintext

\c 27 \v 1 Katika mwanzo wa utawala wa Sedekia mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda, neno hil lilimjia Yeremia kutoka kwa Yahwe. (Ingawa nakala nyingi za Kiebrania zinasema "Yehoyakimu, matoleo mengi ya kisasa yanasema "Sedekia", kwa sababu tukio katika sura hii lilitokea katika kipindi cha utawala wake). \v 2 Hiki ndicho Yahwe alisema kwangu, "Tengeneza vifungo na nira kwa ajili yako mwenyewe. Ziweke shingoni mwako. \v 3 Kisha akawatuma kwenda kwa mfalme wa Edomu, mfalme wa Moabu, mfalme wa watu wa amoni, mfalme wa Tiro, na kwa mfalme wa Sidoni. Watume kwa mkono wa wajumbe hao wa wafalme ambao walikuja Yerusalemu kwa Sedekia mfalme wa Yuda. \v 4 Toa amri kwao kwa ajili ya mabwana zao na sema, ' Yahwe wa majeshi, Mungu wa Israeli, anasema hivi: Hivyo ndivyo mtakavyosema kwa mabwana zenu,