sw_jer_text_reg/41/01.txt

1 line
643 B
Plaintext

\v 1 Lakini ilitokea kwamba katika mwezi wa saba Ishmael mwana wa Nethania mwana wa Elishama, toka familia ya kifalme, na maafisa baadhi wa mfalme, walikuja - wanaume kumi walikuwa pamoja naye - kwa Gedalia mwana wa Ahikam, huko Mizpa. Walikula chakula pamoja hukp Mizpa. \v 2 Lakini Ishmael mwana wa Nethania, na wanaume kumi ambao walikuwa pamoja naye waliinuka na kumvamia Gedalia mwana wa Ahikam mwana wa Shafan, kwa upanga. Ishmael alimuua Gedalia, ambaye mfalme wa Babeli alimweka kuwa msimamizi wa nchi. \v 3 Kisha Ishmael aliwauwa Wayahudi wote ambao walikuwa pamoja na Gedalia huko Mizpa na Wakaldayo wanaume wa kupigana kukutwa huko.