sw_jer_text_reg/26/10.txt

1 line
519 B
Plaintext

\v 10 Kisha wakuu wa Yuda wakasikia maneno haya na wakapanda kutoka nyumba ya mfalme kwenda kwenye nyumba ya Yahwe. Wakakaa katika njia ya lango katika Lango Jipya la nyumba ya Yahwe. \v 11 Makuhani na manabii wakasema kwa wakuu wa Yuda na kwa watu wote. Wakasema, "Ni haki kwa mtu huyu kufa, kwa maana ametabiri juu ya mji huu, kama mlivyosikia kwa masikio yenu!" \v 12 Kwa hiyo Yeremia akasema kwa wakuu wote na watu wote, "Yahwe amenituma kutabiri juu ya nyumba hii na mji wake, kusema maneno yote ambayo mmeyasikia.