sw_jer_text_reg/47/01.txt

1 line
399 B
Plaintext

\v 1 Hili ni neno la Yahwe lililokuja kwa Yeremia nabi juu ya Wafilisiti. Neno hili lilimjia kabla Farao hajaishambulia Gaza. \v 2 "Yahwe asema hivi: Tazama, mafuriko ya maji yanainuka huko kaskazini. Yatakuwa kama mto uliofurika! Kisha yataigharikisha nchi na kila kitu ndani yake, miji yake na watu wakaao ndani yake! Kila mtu atapiga kelele ya kuomba msaada, na wakaaji wote wa nchi wataomboleza.