sw_jer_text_reg/44/01.txt

1 line
561 B
Plaintext

\v 1 Hili lilikuwa neno ambalo lilikuja kwa Yeremia kuhusu Wayahudi wote walioishi katika nchi ya Misri, wale wanaoishi Migdoli, Tahpanhesi, Memphis, na katika nchi ya Patrosi. \v 2 "Yahwe wa majeshi, Mungu wa Israel, asema hivi: Wewe mwenyewe umeyaona maafa yote niliyoleta juu ya Yerusalemu na miji yote ya Yuda. Ona, ni ukiwa leo. Hakuna yeyote anaishi mwao. \v 3 Hii ni kwa sababu ya mambo maovu waliyofanya kunikosea mimi kwa kwenda kuchoma ubani na kuabudu miungu mengine. Hawa walikuwa miungu ambao wala wao wenyewe, wala ninyi, wala mababu zenu walijua.