sw_jer_text_reg/43/08.txt

1 line
509 B
Plaintext

\v 8 Basi neno la Yahwe lilikuja kwa Yeremia huko Tahpanhesi na kusema, \v 9 "Chukua mawe makubwa mkononi mwako, na, kwenye macho ya watu wa Yuda, yafiche kwenye chokaa kwenye njia ya kuingia katika nyumba ya Farao huko Tahpanhesi. \v 10 Kisha wakasema nao, "Yahwe wa majeshi, Mungu wa Israel, asema hivi, 'Ona, nimekaribia kutuma wajumbe kumchukua Nebukadreza mfalme wa Babeli kama mtumwa wangu. Nitaweka kiti cha enzi juu ya mawe haya ambayo wewe, Yeremia, umeyazika. Nebukadreza ataweka banda lake juu yao.