sw_jer_text_reg/37/03.txt

1 line
417 B
Plaintext

\v 3 Kwa hiyo Mfalme Sedekia, Yehukali mwana wa Shelemia, na Zefania mwana wa Maaseya kuhani alituma ujumbe kwa Yeremia nabii. Walisema, "Omba kwa niaba yetu kwa Yahwe Mungu wetu." \v 4 Sasa Yeremia alikuwa anakuja na kwenda miongoni mwa watu, kwa kuwa alikuwa bado hajawekwa ndani ya gereza. \v 5 Jeshi la Farao lilitoka Misri, na Wakaldayo waliozingira Yerusalemu walisikia habari kuhusu wao na kuondoka Yerusalemu.