sw_jer_text_reg/35/12.txt

1 line
484 B
Plaintext

\v 12 Kisha neno la Yahwe likaja kwa Yeremia, likisema, \v 13 "Yahwe Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, anasema hivi, 'Nenda na useme kwa wanaume wa Yuda na wakaaji wa Yeruslemu, 'Hamtapokea maelekezo na kulisikiliza neno langu? —hili ni tangazo la Yahwe. \v 14 Maneno ya Yonadabu mwana wa Rekabu aliyowapa wanawe kama amri, wasinywe divai yoyote, yameheshimiwa hadi leo. Wameitii amri ya babu yao. Lakini mimi, nimekuwa nikifanya matangazo kwenu bila kukoma, lakini hamnisikilizi.