sw_jer_text_reg/32/03.txt

1 line
556 B
Plaintext

\v 3 Sedekia mfalme wa Yuda alikuwa amemfunga na kusema, "Kwa nini unatabiri na kusema, 'Yahwe anasema hivi: Angalia, niko karibu kuweka mji huu katika mikono ya mfalme wa Babeli, na atauteka. \v 4 Sedekia mfalme wa Yuda hatapona kutoka kwenye mikono ya Wakaldayo, kwa maana hakika atatiwa katika mkono wa mfalme wa Babeli. Mdomo wake utazungumza kwenye mdomo wa mfalme, na macho yake yatayaona macho ya mfalme. \v 5 Atampeleka Sedekia Babeli, na atabaki huko hadi nimuadhibu—hili ni tangazo la Yahwe. Ingawa unapigana dhidi ya Wakaldayo, hautafanikiwa."