sw_jer_text_reg/24/01.txt

1 line
590 B
Plaintext

\v 1 Bwana alinionyeshea kitu. Tazama, vikapu viwili vya tini viliwekwa mbele ya hekalu la Bwana. (Maono haya yalitokea baada ya Nebukadreza, mfalme wa Babeli, kumchukua mateka Yekonia mwana wa Yehoyakimu, mfalme wa Yuda, maofisa wa Yuda, mafundi na wafua vyuma kutoka Yerusalemu na kuwapeleka Babeli.) \v 2 Kikapu kimoja cha tini kilikuwa nzuri sana, kama tini za kwanza zilizoiva, lakini kikapu kingine cha tini zilizokuwa mbaya sana zisizoweza kuliwa. \v 3 Bwana akaniambia, "Unaona nini Yeremia?" Nikasema, "Tini. Tini ambazo ni nzuri sana na tini ambazo ni mbaya sana haziwezi kuliwa."