sw_jer_text_reg/21/08.txt

1 line
494 B
Plaintext

\v 8 Basi uwaambie watu hawa, 'Bwana asema hivi Angalia, nitaweka mbele yako njia ya uzima na njia ya mauti. \v 9 Mtu yeyote anayeishi katika mji huu atakufa kwa upanga, njaa, na tauni; lakini mtu yeyote atakayetoka na kuanguka kwa magoti mbele ya Wakaldayo ambao wamefungwa dhidi yako ataishi. Yeye ataokoka na maisha yake. \v 10 Kwa maana nimeweka uso wangu juu ya mji huu ili kuleta maafa na sio kuleta mema-hili ndilo tamko la Bwana. Utatiwa mkononi mwa mfalme wa Babeli naye atauteketeza.'