sw_jer_text_reg/16/01.txt

1 line
452 B
Plaintext

\v 1 Ndipo neno la Bwana likanijia, kusema, \v 2 "Usiwe na mke, wala usiwe na wana au binti hapa. \v 3 Kwa kuwa Bwana asema hivi kwa wana na binti ambao wamezaliwa hapa, kwa mama waliowabeba, na kwa baba waliowafanya wazaliwe katika nchi hii, \v 4 'Watakufa vifo vya magonjwa. Hawataliliwa wala kuzikwa. Watakuwa kama samadi juu ya nchi. Kwa maana wataangamizwa kwa upanga na njaa, na miili yao itakuwa chakula cha ndege wa angani na wanyama wa dunia.'