sw_jer_text_reg/34/17.txt

1 line
702 B
Plaintext

\v 17 Kwa hiyo Yahwe asema hivi, 'Ninyi wenyewe hamkunisikiliza. Mlipaswa kuwa mmetangaza uhuru, kila mmoja wenu, kwa ndugu zenu na Waisraeli wenzenu. Kwa hiyo angalia! Niko karibu kutangaza uhuru kwenu—hili ni tangazo la Yahwe—uhuru wa upanga, tauni, na njaa, kwa maana naenda kuwafanya kitu cha ajabu katika macho aya kila ufalme juu ya dunia. \v 18 Kisha nitashughulika na watu waliolivuja agano langu, ambao hawakuyashika maneno ya agano ambalo walilithibitisha mbele zangu walipomkata ng'ombe dume katika vipande viwili na kutembea katika vipande vyake, \v 19 na kisha viongozi wa Yuda na Yerusalemu, matowashi na makuhani, na watu wote wa nchi wakatembea katika vipande vya yule ng'ombe dume.