sw_jer_text_reg/33/12.txt

1 line
432 B
Plaintext

\v 12 Yahwe Mungu wa majeshi asema hivi: Katika sehemu hii ya ukiwa, ambamo sasa hakuna mwanadamu wala mnyama—katika miji yake yote kutakuwepo tena malisho ambapo wachungaji wataweza kupumzisha makundi yao. \v 13 Katika miji hii katika nchi ya vilima, nchi tambarare, na Negevu katika nchi ya Benyamini na kuzunguka Yerusalemu yote, na katika miji ya Yuda, makundi yatapata njia chini ya mkono wa yule anayewahesabu,' asema Yahwe.